Header Ads

VURUGU: MABOMU YA MACHOZI YARINDIMA JIJI LA MWANZA

Jeshi la Polisi Jijini Mwanza,leo June 11, 2014,asubuhi. limelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafanyabiashara wadogo  maarufu  kama  machinga waliokuwa wakipinga kuondolewa katika eneo la Kempu na eneo la soko la Makoroboi jijini Mwanza.

 


Hatua hiyo imesababisha vurugu kubwa na kusimamishwa kwa shughuli mbalimbali za kijamii, ikiwemo kufungwa kwa maduka hadi katikati ya eneo la jiji na baadhi ya huduma ya usafiri kukosekana kwa muda katika barabara zinazokatiza katikati ya jiji  kuanzia saa nne asubuhi .



Kamanda wa Polisi mkoani humo, Valentino Mlowola, amedai  kuwa leo Juni 11, 2014 ,Jeshi hilo limelazimika kutumia mabomu hayo ili kuwatawanya wafanyabiashara hao waliokuwa wakihatarisha amani na kwamba  hakuna mtu yeyote aliyeripotiwa kujeruhiwa katika vurugu hizo.  



 Katika hatua nyingine,Serikali imetakiwa kuingilia kati migogoro ya wamachinga nchini.
Akiomba mwongozo Bungeni mjini Dodoma, Mbunge wa Nyamagana, Ezekiel Wenje, ameitaka serikali kusitisha zoezi hilo ili kutafuta njia mbadala ya kushughulikia migogoro kati ya serikali na wamachinga.
Naye Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, amesema kuwa Serikali inashughulikia suala hilo ili kubaini ukweli na itatoa taarifa Bungeni baada ya kuhakikisha tukio hilo.

No comments

Powered by Blogger.