Kutoka Zanziber: BOMU LA MISUMARI LAUWA MMOJA ZANZIBAR
Bomu la misumari lauwa mmoja Zanzibar
14 Juni, 2014 - Saa 12:23 GMT
Mtu mmoja ameuwawa huku wengine kadhaa kujeruhiwa katika shambulio la bomu kisiwani Zanzibar.
Baadhi ya waathiriwa walikuwa wanaondoka katika msikiti mmoja ulioko katika maeneo ya mji mkongwe, mjini Zanzibar.
Haijulikani ni nani aliyefanya
shambulio hilo ambalo lilijiri mkesha wa sherehe za kimataifa za filamu
katika kisiwa hicho; na piya wakati kuna kongamano ya viongozi wa dini
ya Islamu katika Afrika Mashariki, likifanyika huko.
Mwandishi wetu nchini Tanzania amezungumza na
Insepekta Mkuu wa Zanzibar, Mohammed Mhina, ambaye amemwambia kuwa bomu
liloripuka lilikuwa na misumari.
Hilo ni shambulio la pili la bomu mwaka huu.
Mwezi February mabomu mawili tofauti
yaliripuliwa nje ya kanisa Anglikana, mji mkongwe, pamoja na mkahawa
uliokuwa karibu na kanisa hilo.
Kumekuwa na hali ya wasiwasi wa kidini katika kisiwa hicho.
ANGALIA PICHA INASIKITISHA; BOMU LALIPUKA DARAJANI ZANZIBAR, MMOJA AFARIKI
Mlipuko unaosadikiwa kuwa ni bomu jana Juni 13, 2014 ulilipuka eneo la Darajani Zanzibar na kusababisha kifo cha mtu mmoja na kujeruhi watatu.
Tarifa
zinasema mlipuko Huo umetokea baada ya waumini wa dini ya kiislamu
kumaliza muhadhara uliokuwa ukitolewa Miskiti wa darajani baada ya salsa
ya Isha.
Aliyekufa
ni mmoja kati ya wahadhiri waliokuja kutoka Tanga na Sheikh Hamad ndiyo
aliyekuwepo theater. Na Sheikh Kassim Mafuta kaumia kidogo.
Majeruhi 3
wamelazwa hospitali ya Mnazi Mmoja, Zanzibar wakiwa na majeraha madogo
'madogo. Majeruhi wa nne yupo theatre sasa hivi na nali yake sio mbaya
Post a Comment