UNAAMBIWA TANZANIA NI NCHI YA PILI KWA MATUMIZI YA SMARTPHONES
Jumamosi, Juni 14, 2014
TANZANIA imetajwa kuwa nchi ya pili katika nchi za Kusini mwa Jangwa
la Sahara, kwa manunuzi na utumiaji wa simu za smartphone ikitanguliwa
na Afrika Kusini.
Mkurugenzi wa kampuni ya bidhaa ya Puku, Meck Mbwana, alibainisha
hayo jijini Dar es Salaam juzi wakati wa hafla ya uzinduzi wa kifaa
hicho ambacho hutumika katika kuchaji simu za aina hiyo.
Alisema jambo hilo ndiyo sababu kubwa iliyowafanya kutambulisha Puku
katika nchi hii kwa bara la Afrika, ambapo awali walilenga kuuza katika
masoko ya Ulaya, hususani Marekani.
Alisema sababu nyingine ni kuweka uzalendo mbele, kwani asilimia 75
ya umiliki wa kampuni hiyo ni Watanzania huku asilimia 25 ikiwa ni
Wamarekani.
Rais wa Puku Tanzania, Joseph Sikare, alisema pamoja na kuwepo kwa
kifaa kama hicho kinachotengenezwa na makampuni mengine, wao wamekuja
tofauti kwa kutengeneza kitu chenye ubora zaidi, mvuto kimuonekano na
kinachodumu kwa muda mrefu.
Balozi wa Puku, Happiness Magese, aliwataka Watanzania kuwaunga mkono
Puku, kwa maelezo kuwa wanatangaza utalii wa Tanzania duniani kupitia
kifaa hicho ambacho jina lake ni aina ya mnyama wa swala anayepatikana
Tanzania pekee.
Post a Comment