SACCOSS: MAMA SALMA KIKWETE AWEKA JIWE LA MSINGI LA OFISI YA TEWO SACCOS-TEMEKE
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akiwapungia wananchi waliohudhuria sherehe
za uwekaji wa jiwe la msingi la TEWO Saccos huko Temeke tarehe 17.6.2019Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea zawadi ya picha kutoka kwa Mjumbe
wa Bodi ya TEWO Saccos Mama Catherine John (Bi Nyakomba) wakati wa
sherehe za uwekaji wa jiwe la Msingi la Saccos hiyo huko Temeke tarehe
17.6.2014.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea Tuzo maalum kutoka kwa Mwenyekiti
wa TEWO Saccos Ndugu Sophia Kinega. Mama Salma alipewa Tuzo hiyo kwa
ajili ya ushirikiano wake na Saccos hiyo katika kuchangia kwa kiasi
kikubwa ujenzi wa jengo la ofisi ya TEWO Saccos.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akiwahutubia wanachama wa TEWO Saccos, mwana
Vicoba na wananchi wa wilaya ya Temeke waliohudhuria sherehe ya uwekaji
wa jiwe la msingi la ujenzi wa ofisi za TEWO Saccos huko Temeke tarehe
17.6.2014.Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akimkabidhi cheti Ndugu Yusuf Manji
kilichotolewa na TEWO Saccos kwa watu na makampuni mbalimbali
yaliyoshiriki katika kuchangia ujenzi wa jengo la TEWO Saccos huko
Temeke tarehe 17.6.2014.Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akimkabidhi cheti (Certificate of
Appreciation) Ndugu Philomena Marijani, Afisa kutoka Taasisi ya Wanawake
na Maendeleo,WAMA, kilichotolewa na TEWO Saccos kwa ajili ya
kuwashukuru watu na Taasisi mbalimbali zilizochangia kwa kiasi kikubwa
ujenzi wa ofisi za Saccos hiyo huko Temeke tarehe 17.6.2014.Mwakilishi
wa Kampuni ya Mabasi ya Usafiri Dar es Salaam, UDA, Ndugu Simon
Bulenganiya akikabidhi mfano wa hundi ya sh 30,000,000 kwa ajili ya
ujenzi wa Ofisi ya TEWO Saccos kwa Mwenyekiti wa Saccos hiyo Ndugu
Sophia Kinega wakati wa sherehe ya uwekaji wa jiwe la msingi terehe
17.6.2014.Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akipata maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa
jengo la ofisi ya TEWO Saccos wakati wa sherehe ya kuweka jiwe la msingi
huko Temeke tarehe 17.6.2014.Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akiweka jiwe la msingi la ujenzi jengo la
ofisi ya TEWO Saccos kwa kufungua kitambaa katika sherehe iliyofanyika
wilayani Temeke tarehe 17.6.2014. Kushoto kwa Mama Salma ni Mwenyekiti
wa UWT Mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Janneth Masaburi.Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa
TEWO Saccos na wale wa serikali waliohudhuria sherehe ya uwekaji wa jiwe
la msingi la SACCOS hiyo tarehe17.6.2014.
Post a Comment