Home
/
Unlabelled
/
USALAMA: WATU WATATU WATIWA MBARONI MKOANI PWANI,WAKUTWA NA BASTOLA NA SARE ZA JESHI
USALAMA: WATU WATATU WATIWA MBARONI MKOANI PWANI,WAKUTWA NA BASTOLA NA SARE ZA JESHI
Kamanda
wa Polisi mkoani humo Kamishna Mwandamizi Msaidizi wa Polisi (SACP)
Ulrich Matei akionyesha silaha na mavazi ya kijeshi waliyokamatwa nayo
Watuhumiwa hao.
Na John Gagarini, Kibaha
JESHI
la Polisi mkoani Pwani limefanikiwa kuwakamata watu watatu akiwemo mtu
Daniel Mtalisi mkazi wa Kisemvule wilaya ya Mkuranga ambaye alipitia
mafunzo ya kijeshi kwa tuhuma za kufanya tukio la uhalifu wa kupora
silaha na vitu mbalimbali.
Mtuhumiwa
huyo ambayealiwahi kupata mafunzo ya kijeshi kwenye Jeshi la Kujenga
Taifa (JKT) kikosi namba 833 Oljoro Arusha na namba yake ni MT. 95150.
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo kwa waandishi wa habari mjini Kibaha, kamanda wa
Polisi mkoani humo Kamishna Mwandamizi Msaidizi wa Polisi (SACP) Ulrich
Matei alisema kuwa tukio hilo lilitokea Juni 17 mwaka huu majira ya saa
2 usiku huko Kijiji cha Kisemvule kata ya Vikindu kata ya Mkuranga
wilaya ya Mkuranga.
Kamanda
Matei alisema kuwa watuhumiwa hao wengine wakiwa ni Khalfan Abas (25)
mkazi wa Mwanambaya na Mashaka Masanja (24) mkazi wa Mwongozo Kigamboni
Jijini Dar es Salaam walikamatwa baada ya polisi kufanya msako mkali na
kumkuta mtuhumiwa huyo akiwa na silaha hiyo ambayo walimpora Musa
Kambangwa ambaye ni mfanyabiashara wa Mwanambaya.
“Watu
hao walimvamia mlalamikaji ambaye alikuwa akirejea nyumbani kutoa
kwenye biashara zake walimteka kisha kumpiga na walimwamuru awapeleke
nyumbani kwake na kuichukua silaha hiyo bastola yenye namba A 569542
aina ya Browning, Carriber 7.65 mm, magazine 2 na risasi 23, chaja 1
ambavyo alikuwa amehifadhi nyumbani kwake,” alisema Kamanda Matei.
Aidha
Kamanda Matei alisema kuwa kabla ya kukamatwa watuhumiwa hao walifanya
tukio hilo Juni 11 mwaka huu huko Kijiji cha Mwanambaya ambapo
walimvamia mlalamikaji akiwa na mke wake.
“Walimjeruhi
kwa kutumia silaha mbalimbali za jadi na kumsababishia maumivu makali
kisha kumtaka awape funguo ya nyumba yake ili waingie ndani lakini
alikataa wakaendelea kumpiga hadi alipopoteza fahamu na kuichukua funguo
na kuingia ndani na kuchuakua silaha hiyo na simu 2 aina ya Nokia,
Inveta , deki 1 ya Dvd na viatu pea moja kisha kutoweka na ndipo
walipokuja kukamatwa Juni 17,” alisema Kamanda Matei.
Alisema
kuwa baada ya tukio hilo ndipo walipofanya msako na kufanikiwa kuvikuta
vitu hivyo ambapo mtuhumiwa wa kwanza alikutwa na sare za Jeshi.
Alibainisha
kuwa mlalamikaji anaendelea vizuri na kuwataka watu kutoa taarifa za
uhalifu ili kuzuia matukio hayo ambayo yameanza kuibuka kwa wingi na
watuhumiwa hao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani mara upelelezi wa
tukio hilo utakapokamilika.
Post a Comment